You are currently viewing Tofauti ya mabati gauge 28 na gauge 30

Tofauti ya mabati gauge 28 na gauge 30

Ni muhimu kutumia bati zenye ubora katika uezekaji wa nyumba.
Mara nyingi bati za geji kubwa ni nzuri kutumika katika paa zenye slope ndogo ili panapotokea ukarabati juu ya paa zisibondeke pondeke.

Bati za geji kubwa (G28) hudumu kwa muda mrefu kwa maana ya kuimili hali zote za mvua na jua na si rahisi kupata kutu kwa muda mfupi.
Bati za geji ndogo (G30,G32) ni nzuri kwa majengo ya kawaida ya muda au uzio kwenye majenzi makubwa, na hutumika sana kwenye nyumba zenye slope kali zisizohitaji kupanda juu ya paa.
Na ni muhimu kuyapaka rangi ya kuzuia kutu /kununua yenye kuwa na rangi ya kuzuia kutu.
Ili bati lidumu ni lazima kench/trusses na purlins(mbao zenye kushika Bati) zake ziwe imara haijalishi ni geji ipi unatumia.

Kench na purlins ni vitu muhimu sana vya kuzingatia katika uezekaji wa paa.
Unapotumia bati za geji ndogo ni lazima kenchi na purlins ziwe nyingi ili kuimalisha paa na kuweka muonekano mzuri wa kutokubonyea bonyea.
Kuhusu gharama ni kuwa :-
Gharama za kutumia G28 ni sawa sawa na G30 kwa kuwa malighafi za kuezeka G30 ni nyingi kuliko G28 zenye malighafi ndogo lakini bati zake ni ghali.

Muhimu :
Ili paa liwe na muonekano mzuri ni lazima kuwatumia wataalamu wa majenzi ikiwezekana kila urefu wa bati husika ujulikane na kiwanda kikate urefu husika kuliko kuunga uunga vipande vya either (2.5-3.0m).
Lakini pia ni vizuri uezekaji wa paa uzingatie volume ya maji ili kudesign slope nzuri isiyowezesha maji kutuama na kusababisha kutu.
Hata hivyo ni vema kuanza kufikiria uezekaji wa zege kwa baadhi ya majengo, ambapo finishing yake juu ya paa ifanywe kwa kutumia malighafi zisizo pitisha maji (epox coating n. k……)

je? Unahitaji mabati original yanayodumu bila kupauka, kupata kutu na kuvuja vizazi hadi vizazi kutokea kiwandani moja kwa moja kwa gharama nafuu sana na unaponunua mabati kutoka kwetu usafiri ni bure mikoa yote ndani ya nchi weka oda yako sasa tunakuletea popote ulipo wasiliana nasi kupitia 0656078230 au 0746113477

Leave a Reply