ELIMU KUHUSU MABATI

ELIMU KUHUSU MABATI

Katika miaka ya hivi karibuni mabati yamekuwa yakitumika zaidi katika kuezekea katika nchi za Afrika.Umuhimu wake unatoa sababu za kutosha ya wanaotaka kujenga kujifunza kwa kina kuhusu mabati na namna ya kuchagua.
Mabati hutengenezwa kutokana na metali mbalimbali ikiwemo chuma,aluminium,zinc,kopa ama mchanganyiko kati ya metali mbalimbali ambao hujulikana kama aloi(Alloy)
Alloy hutumika kupunguza eitha udhaifu Fulani ama kupunguza gharama ya kutengeneza bati.Mfano bati linalotengenezwa kwa aluminium pekee ni imara zaidi na halipati kutu,lakini ni gharama sana.Hivyo kupunguza gharama,huongezwa madini ya chuma ama zinc ama tin.
Mfano mwingine ni kwamba mabati yanayotengenezwa kwa chuma na zinc hupata kutu mapema,hasa sehemu zenye unyevu mwingi na chumvichumvi hivyo kiwango cha kimojawapo kati ya zinc na chuma kipunguzwe kudhibiti.
Ni muhimu kujikumbusha yafuatayo:-
2. Aluminium haishiki kutu,inadumu hivyo mabati yaliyotengenezwa kwa 100% aluminium yana ubora .Bei yake ni kubwa ukilinganisha na mabati yatokanayo na chuma ama mchanganyiko wa chuma na madini mengine.
3. Aluminum ikitengenezewa bati zinazotumika mikoa ya pwani hudumu Zaidi
4. Pia bati za aluminium zinafaa kwa sehemu zenye unyevu na chumvichumvi ambako mabati ya metali zingine hupata kutu na kuoza
5. Kopa(copper) hutoa mabati yanayoweza kudumu zaidi ya miaka mia moja.Kutokana na kopa kuwa na gharama kubwa ni wachache huweza kununua,na pia viwanda vingi havitengenezi mabati haya kutokana na kukosa wateja.
6. Mabati yaliyotengenezwa kwa kutumia aluminium na zinc huitwa ALU-ZINC.Neno galvanised humaanisha madini yamepakwa kwenye kitu. Mfano chuma kupakwa zinc kuifanya isipate kutu mapema
7. Zinc pia ni madini aghali,hivyo ni nadra kukuta imetumika kutengeneza bati pasipo kuongezwa na madini mengine
8. Mabati yanayoandikwa Coated humaanisha yamepakwa madini mengine kuzuia kutu(tambua kupaka ni tofauti na alloy)
9. Mabati yanayotokana na mabati ya aluminium,zinc na coppey hayahitaji kupakwa madini mengine kwa sababu ya uwezo wa madini hayo kuhimili unyevu na chumvi chumvi
10. Mabati ambayo ni galvanised na galvalume(yaani yatokanayo na mchanganyiko wa chuma na zinc ama chuma na aluminium hayahitaji kupaka trangi juu yake kwa sababu ya mchanganyiko wake ambao ni PRE-COATED

11. Mabati ambayo ni coated yaani yaliyopakwa rangi juu yake,ni muhimu kuhakikisha rangi iliyotumika ni ile itokanayo na mimea kama Kynar 500 tofauti na yale ambayo hupakwa rangi za Acrylic
GAUGE/GEJI
Wengi tumekuwa tukisikia neon geji lakini tusijue maana yake.
Unapozungumzia geji unazungumzia nkina cha bati (yaani Unene wa bati)Bati inapotengenezwa kiwandani,mchanganyiko wake huthibitiwa kwenye kipimo kinachohakiki mchanganyiko unakuwa na kina(unene) unaotakiwa
Kipimo kinachopima unene wa bati husomeka katika namba ndogo bati linapokuwa nene,mfano geji namba 26 ni nene kuliko geji namba 28 nani nene kuliko geji namba 30.Hivyo bati nene ni geji namba 26.
Unene wa bati una uhusiano mkubwa na ubora.Bati geji namba 26 ni bora zaidi kuliko namba 28.Bati geji namba 28 ni bora kuliko namba 30.
Kadiri unene unavyoongezeka ndivo madini ya aluminium huwa mengi zaidi hivyo unapoenda kuchagua bati chagua geji yenye namba ndogo zaidi kama 26,28.
Bei ya geji namba 26 kwa madini yaleyale ni kubwa kuliko namba 28
Bati nyingi huanza gauge 22(22GA)
Mabati yanapotengenezwa hutoka yakiwa hayana mikunjo.Huwa yamenyoka.Kisha huwekwa mikunjo ili kulifanya kuwa imara(lisilokunjikakunjika).Hapo huitwa corrugated,yaani lina mikunjo/migongo
IT 4/IT5
Wengi pia wamekuwa wakiuliza maana ya maneno haya IT5/IT6
Neno IT huwakilisha Industrial Trough,yaani kwa kifupi ni sawa na kusema mikunjo.Inapokuwa na mikunjo 4 huitwa IT4,inapokuwa 5 inaitwa IT5.
WASILIANA NASI    0656078230

Leave a Reply